Bwana Yesu asifiwe tunawamshukuru wale wote waliotembelea ukurasa wetu na blog hii ya KILIMANJARO HOUSE OF PRAYER,
Tunapenda
kuwataarifu kwamba hili sio kanisa bali ni mahali tu tumejitolea ili
tuweze kukutanika kwa ajili ya maombi na si vinginevyo, Tunajua umuhimu
wa maombi katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote anayeishi duniani
hivyo kwa Mwongozo wa ROHO MTAKATIFU ndio tukaona tushirikishane jambo
hili la Baraka katika maisha ya kila siku duniani.
Jambo
hili limekuwa jema na Mungu atupaye uwezo wa kufanya makuu siku zote
atusaidie sote ili shetani asituvuruge wala kuleta uhasama kati ya
madhehebu na makanisa.
Tuongozwe
na Roho kama Neno la MUNGU wetu linavyotuagiza katika WAGALATIA 5:25,
na WAEFESO 6:10-12, jambo lililo jema watumishi wa Mungu tuelewane na
tumpinge shetani na zaidi sana tusikamane kuujenga mwili wa Kristo Yesu
Bwana wetu na tukizidi kuombeana kwa kusudi la kuwakamilisha WATAKATIFU
ambalo ndilo hasa lengo la Mungu kwa kanisa.
MUNGU WA MBINGUNI AZIDI KUWABARIKI
KILA MMOJA NA KUMPA KILA MMOJA HEKIMA YA KUTENDA SAWA NA NENO
LINAVYOTUAGIZA KATIKA BIBLIA, ILI SIKU MOJA TUKAPEWE TAJI TUKIWA
MASHUJAA TULIOSHINDA VITA VYA KIROHO HAPA DUNIANI.
Endeleeni kutembelea ukurasa wetu na pia mtoe maoni kile ambacho kitakuwa chema zaidi kwa kusudi la Ufalme.AEN.