Watu
wengi tunajua ya kuwa MUNGU
alituumba ili tumilki na kutawala. Kitu
kilicho sababisha hata sasa hatufanikwi ni kule kutotii sauti ya MUNGU na jambo hili limefanya watu
kutosonga mbele kimaisha maana neno la MUNGU
linasema katika Joshua 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku upate kuangalia na kutenda sawaswa na maneno
yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo utakapofanikisha
njia yako kisha ndipo utakapostawi sana.
Je
ndani yako ndani yako kunalo neno la Mungu? Wakristo wengi wamejisahau hata
kusoma neno la MUNGU, unakuta
mkristo muda mwingi yuko WhatsAp, Facebook, wasengenyaji n.k. Na watu hawa ndio
mara nyingi utawaona wako rohoni kumbe hao ndio waharibifu wa kazi ya MUNGU. Watu wengi wanajikuta wamewaamini hawa watu na kuwapa mambo yao ya siri halafu wanayakuta yamezagaa mitaani wasijue kua Siri
zao wamepeleka sehemu isiyo sahihi. Sababu kuwa mwana wa MUNGU
nikuwa mbeba siri za MUNGU kwa hiyo
watu hawa wamekuwa kidonda katika kazi ya Mungu na hii imekua ikurudisha nyuma
kazi ya MUNGU.
Na watu hawa wamekuwa wakipatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchungu wa
ndani (yaani lile jambo ulilolibeba moyoni ). Biblia inasema MITHALI 14:30a Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili . Je hawa
wapendwa feki wanaua watu wangapi kwenye makanisa wanayosali? Kama na wewe upo
katika kundi hilo tambua biblia inasema katika Luka17:2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni
mwake, akatupwe baharini, kuliko
kumkosesha mmoja wa wadogo hawa. Je kunayo sababu ya wewe kusema kuwa nimeokoka!
badilika tambua kuwa unavyofanya MUNGU
hapendezwi na wewe na shetani anakushangaa.
Tambua
kuwa bado unayo nafasi ya kutengeneza na Bwana MUNGU wako, nenda mbele za MUNGU mwabie baba nimekosa tamka makosa
yako bila kuficha mbele za MUNGU
sababu Mithali 11:7 inasema Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; na
matumaini ya uovu huangamia. Kwahiyo inapasa kuungama dhambi zote.Wala Usiache
hata moja kwa kuhofia watu wanasikia
endelea kumsihi MUNGU wako naye
atakusamehe.
Ukisoma
ZABURI 51:7 Unisafishe kwa hisopo
nami nitakuwa safi, Unioshe, nami
nitakuwa mweupe kama theluji, hii ina maana kwamba dhambi zako zitakuwa mbali
na wewe na wakati huo utaanza kuisikia
sauti ya MUNGU ikikuongoza katika Jina
lipitalo majina yote, jina la YESU.
MUNGU AWABARIKI KWA KUWEZA KUTUMIA MUDA WAKO
KUJIPATIA UFAHAMU KATIKA NENO LA MUNGU
MTUMISHI FRANK MINJA.